Posts

Showing posts from April, 2022

01. MUNGU WA MAPENDO

MUNGU WA MAPENDO (By Rose Muhando) [Nini kitanitenganisha ( Na upendo wa Mungu Baba), Ikiwa ni dhiki au njaa (Havitananitenga naye Baba), Mauti, upanga, na dhihaka (Havitananitenga naye Baba) ] x2 Chorus: [Sina hofu sibabaiki, Kwake yeye nime/nitashinda, Milele yote nime/nitashinda, Tena zaidi ya kushinda, Kwake yeye aliyenipenda] x2 Kwenye zamu yangu nitasimama,  Kwa miguu yangu nitasimama, Nione Bwana atakavyonijibu mimi, Kwa habari ya kulalamika kwangu, Bwana aliniambia neno hili, “Usiogope maneno yao, Usitetemeke mbele yao, usifadhaike mbele yao, Maana imeandikwa, kwa ajili yako ninauawa, kama kondoo wa kuchinjwa, kifo nimehesabiwa, Kifo nimehesabiwa, mimi sibabaiki. Bridge: Shetani usinisumbue (Shetani usinisumbue) Wala usinibababishe (Wala usinibababishe)  Funga kinywa ukatoweke (Funga kinywa ukatoweke)  Nyamaza kimya ukapotee (Kwa jina la Yesu ukatoweke)  Nyamaza kimya ukapotee (Nyamaza kimya ukapotee). Chorus: [Sina hofu sibabaiki, Kwake yeye nime/nitashind...

02. NIBEBE

NIBEBE (By Rose Muhando) Chorus: Nibebe nibebe nibebe nibebe, Nibembeleze nibebe, Nichukue unibebe, Mikononi mwako niwe salama. Verse 1: E mungu angalia kunena kwangu,  Na usikie sauti ya kilio changu, Moyo wangu umechoka sana baba,  Kwa ajili ya wingi wa mateso yangu, Nafsi yangu imegandamana na mavumbi, Niokoe mikononi mwa midomo ya mbwa, Kwanini ninateswa sana kwa ajili yako babangu? Niokoe mikononi mwa watu wabaya, fanya hima unisaidie nibebe. Chorus: Nibebe nibebe nibebe nibebe, Nibembeleze nibebe, Nichukue unibebe, Mikononi mwako niwe salama. Nimechoka peke yangu safari ngumu ni ndefu nibebe. Chorus: Nibebe nibebe nibebe nibebe, Nibembeleze nibebe, Nichukue unibebe, Mikononi mwako niwe salama. Verse 2: Macho yangu yamedhoofukwa machozi, Kwani mateso yangu hayapimiki kwa mizani, Kwa kuwa aliyenitukana siye adui yangu, bali ni rafiki yangu tuliyejuana naye sana, Tulikula pamoja, tulisali pamoja, kanisani pamoja, Bwana asifiwe kwa sana, Kumbe mwenzangu alikusudia kuniangami...

03. NYOTA YA AJABU

NYOTA YA AJABU (By Rose Muhando) Verse 1: Ile nyota ya ajabu, yaonekana mashariki Imejaa ishara zote, za kuzaliwa mfalme Mamajuzi wako nyuma, kuifuata nyota ile walifika Yerusalemu, nao wakauliza (Repeat) Yuko wapi yeye aliyezaliwa, mtawala wa wayahaudi ili tumsujudie. Chorus: Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi Atakayewaokoa watu na dhambi zao Dunia shangilieni, amezaliwa messiah Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana. Verse 2: Walikuwako na wachungaji, waliokaa makondeni Wakilinda kundi lao kwa zamu usiku Malaika kawatokea, kawambia msiogope Maana leo katika Yuda, amezaliwa messiah. Chorus: Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi Atakayewaokoa watu na dhambi zao Dunia shangilieni, amezaliwa messiah Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana. Verse 3: Walipokwisha kusema haya, Malaika wa bwana Waliimba wimbo ule, wimbo usio na mwisho Utukufu juu kwa Mungu mbinguni Duniani we amani kwa aliowaridhia. Chorus: Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi Atakayewaokoa watu na dhambi zao Dunia shangilieni, a...

04. SITANYAMAZA

SITANYAMAZA (By Rose Muhando) Eeeehhhh! Mimi Mungu (Me, God) Matendo nitalia, Kwa sinani nitaomboleza Sodoma nitanung'unika, Mipakani nitashambulia Mijini wameniacha,Kila mara nitashambulia Maisha ya wanadamu, Yamenichosha! Oh oh mimi Sitanyamaza, wala sitanyamaza Lakini nitalipa ujira wa vifuani mwao Maovu yenu ninyi, pamoja na baba zenu nasema nitalipa ndio mjue mimi ni Bwana Mmefukiza uvumba, na kunitukana Kwa ajili ya haya mtajutia vitani mwenu? (repeat) Mmefanya uzinzi katikati ya milima Usiku wa manane mmefanya ukahaba Kwenye njia kuu na vichochoro mmefanya mapatano Kwenye mialoni na mipera mmefanya machukizo. (repeat) Ulitumaini uzuri wako ukafanya ukahaba Kila kijana aliyepita ulimwona anafaa Awe mzuri na sura mbaya ulifunua marinda. Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda Wako wapi mapenzi zako mbona sasa unakonda Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda Wako wapi waelizamu (?) wako mbona sasa unakonda. Miji mizuri imekuwa ukiwa Majumba mazuri yamefungwa kabisa Wana w...

05. UTUKUZWE

UTUKUZWE (By Rose muhando) Ee Mungu utukuzwe, milele na milele, Tena uinuliwe, katika mataifa yote, Ee Mungu utukuzwe, milele na milele, Ee Mungu uinuliwe, milele na milele, Tena uhimidiwe katika mataifa yote, Jina lako la ajabu, Wewe utishaye kuliko x2 Wala haufanananishwi na chochote, Jina lako Baba la ajabu. Refrain: Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika), Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia), Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania) Wakafika (Kule Kanaani salama) x2 Usifiwe, utukuzwe x2 Utukufu ni wako, milele na milele x2 Haya visiwa na viimbe,  Mito na ipige makofi, Ndege na waseme amina kubwa, Wanyama wa mwitu wasifu x2 Bwana anatawala/Maana unatawala, wewe Bwana, Heshima na enzi ni vya Bwana, Utukufu na nguvu ni vya Bwana, Umeketi mkono wenye nguvu  x2 Refrain: Wewe uliupiga mwamba  (maji yakabubujika), Katikakati ya jangwa  (wewe ulifanya njia), Walipokumbana na adui  (Wewe uliwapigania) Wakafika  (Kule Kanaani salama)  x2 Usifiwe, ut...

06. KIATU KIVUE

KIATU KIVUE (By Rose Muhando) Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue, Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue, Ulichotoka nacho kwa farao nakwambia, Pahali hapa ni patakatifu hicho kiatu kivue (x2) Musa hicho kiatu, Musa hicho kiatu, Nataka ninene nawe, nataka nikutumie, Nataka nikuinue, nataka nikubariki, Watu wangu waangamia,taifa langu la Israeli, Watu wangu wanasononeka,watu wangu wanateseka, Nataka nikutumie wewe, ukaokoe taifa langu we. Hata leo mungu anena nasi hicho kiatu we, Kiatu ni dhambi uzifanyazo ninakwambia, Ukahaba unaoeneza kando kando ni kiatu, Wivu na masengenyo vimekuja ni kiatu, Kitakupeleka jehanamu hicho kiatu, Kitakupeleka motoni wewe hicho kiatu, Uzinzi unaoeneza wewe ni kiatu, Uvalie wake wa wenzio magoti we nakwambia, Utongoza waume wa wenzio ni kiatu we, Kitakupekea jehanamu hicho kiatu, Mama hicho kiatu, baba hicho kiatu, Nataka ninene nawe, maana ninakupenda, Nataka ninene nawe, ili nikuokoe, Mimi sitaki uangamie, mimi sitaki upotee, Mimi sitaki uanga...

07. NAKAZA MWENDO

NAKAZA MWENDO (By Rose Muhando) Verse 1: Nafurahia mateso yangu, nafurahia mateso yangu, Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba, Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba. Chorus: Nakaza mwendo, nifike Mbinguni, Nayakabidhi, maisha kwa Bwana, Nauone, uzuri wa bwana x2 Taabu na matatizo, hakuna, Kiu wala njaa, hakuna x2 Verse 2: Lakini mji ule taa yake, ni mwana kondoo, Milele mji ule hauitaji, jua wala mwezi. Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida. Chorus: Nakaza mwendo, nifike Mbinguni, Nayakabidhi, maisha kwa Bwana, Nauone, uzuri wa bwana x2 Verse 3: Lakini waongo na wazinzi, hawataingia, wala waabudu sanamu, hawataingia x2 Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida. Chorus: Nakaza mwendo, nifike Mbinguni, Nayakabidhi, maisha kwa Bwana, Nauone, uzuri wa bwana x2

08. MUNGU WANGU

MUNGU WANGU (By Rose Muhando) E mungu wangu mimi ninatukushukuru, Mbele ya mataifa mimi nitaimba, Dunia nzima nayo itambue hilo, Kwamba jina la yesu pekee ndilo, Ulimwengu mzima uokolewe kwalo. Asubuhi na mapema, mimi nitaimba, Kabla ya kinywa kunena, kwako nitaimba, Tufani ijapozidi wo, kwako nitaimba, Nijapoteswa kabisa, kwako nitaimba, Nijapodharauliwa, kwako nitaimba. Chorus: Swiyi! Sikia e kinanda, Swiyi !  Amka we kinubi, Swiyi !  Sikia e kinanda, Inuka e zumari, inuka kwa sauti (x2) Woo na utukuzwe Mungu, Woo na utukuzwe Mungu,  Yee Jehova adonai, Yee Jehova adonai, El gibo shalom mungu unaitika  El gibo shalom mungu unaitika. Uniondolee majivuno, komesha kiburi, Utawale akili zangu, Bwana niongoze, Unifundishe roho yangu habari za mbingu, Sikizeni eh kizazi changu, Mungu anaishi, Uniondolee majivuno, komesha kiburi, Utawale akili zangu, Bwana niongoze, Unifundishe roho yangu habari za mbingu, Sikizeni eh kizazi changu, Mungu anaishi. Chorus: Swiyi! Sikia e ki...

09. NALEGEA

NALEGEA (By Rose Muhando) {Nalegea, wacha nichakae nje, Lakini utu wangu wa ndani wa fanywa upya}x2 {Dhiki yangu ni nyepesi na ya muda, Yaani fani wa utukufu wa milele} x2 {Nayahesabu mambo yote bure, Kwa ajili ya jina la Yesu (Kristo)} x2 {Natazama, tena imeandikwa, Ni mizuri kama nini – miguu yao} x2 {Wale wote wapelekeo habari njema, Ya utukufu wa Yesu Kristo Bwana wangu} x2 {Nayahesabu mambo yote kama mavi/bure, Kwa ajili ya uzuri wa Yesu (Kristo)} x2 Vipi mwenzangu, wanitazama? Ninaposema habari zako, Ninapotaja na mambo zako, Wacha Makali, hasira nyingi, {Wazielekeza juu yangu, bila sababu, Na kumbe mimi ni mtumishi, niliyetumwa} x2 Nikikwambia uache dhambi, Ushirikina, uchawi fitina, Wanichukia, wanichukia, {Lakini Bwana asema hivi, ni ole wenu, Wanawake washonao hirizi viunoni mwao, Wanaoroga kwa mafumbo, wasio na haya} x2 {Sikia, ewe mkaidi,  Ee mwenye shingo ya chuma, Utavuna ulichopanda,  Mabaya yatakupata} x2 {Kumbuka ewe mshirikina: Uzao wa mwanamke mchawi, Mume...

10. NIPISHE NIPITE

NIPISHE NIPITE (By Rose Muhando) Verse 1: Nakuuliza shetani umepata wapi mamlaka, Ya kukamata akili za watu, Wewe umeleta balaa umeingia makanisani, Umekamata wababa wanabaka watoto wao, Umekamata vijana umewatwika ulevi, Bila kusahau kina mama, vikao vya masengenyo, Sasa nimechoka na mambo yako, Ewe shetani, nipishe nipite. Chorus: Wewe ulimwasi mungu, nipishe nipite, Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite, Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako, Wewe ulimwasi mungu, nipishe nipite, Uliwadanganya Adamu na Eva, songea nipite, Dunia nzima imeharibika, kwa ujanja wako, wewe shetani unaambiwa, mwenyeji wa kuzimu, Sasa nipishe nipite. Verse 2: Hebu nipishe nipite, ninachelewa njiani, Yesu yu karibu kurudi, kulichukua kanisa, Kanda unayo nionyesha yote yamepitwa na wakati, Huna ujanja, Kumbuka miaka elfu mbili iliyopita zamani, Yesu aliposhuka kuzimu, akakunyanganya funguo, Funguo za mamlaka, Nasema nimechoshwa na mambo yako, Wewe shetani nipishe nipite. Chorus: Wewe ulimwasi mungu, ni...

11. UNASHANGAZA

UNASHANGAZA (By Rose Muhando) Tu-ru tururu tu-ru (?) Matendo yako ya ajabu, yashangaza, Fadhili zako za milele Baba, zashangaza, Nikitazama ulivyoumba, ya shangaza, Upendo wako kwangu mimi, yashangaza, Miijuza na maajabu tele, washangaza, Wanyama wa kondeni Baba, washangaza, Milima na mabonde inaimba, washangaza, Wanyama nao wanasema wewe washangaza, Uumbaji wako Mungu, washangaza. Matendo yako ya ajabu, washangaza, Fadhili zako za milele Baba, zashangaza, Uwezo wako kwa ulimwengu, washangaza, Uumbaji wako wa pekee, washangaza, Nikupe nini Mungu wangu? Washangaza, Unavyonipigania Baba, washangaza, Neema zako kwangu mimi, yashangaza. Refrain: Ni wewe, ni wewe, Mataifa waimba, niwewe, Mbingu zaimba, ..?.. imba, Jerusalemu waseme, Mwenye nguvu ni wewe, Mwenye uwezo ni wewe, Wateule na waimbe, ..?.. imba, ..?.. imba, Wateule imbeni, Mwenye nguvu ni wewe, Mwenye uwezo ni wewe, Mwenye mamlaka, Mungu nani kama wewe?

12. UTAMU WA YESU

UTAMU WA YESU (By Rose Muhando) Lile lile, Acheni muone utamu wa Yesu we, Mama we onjeni utamu wa Yesu we, Mwenzenu nimeonja utamu wa Yesu we, Usione nina raha nimeonja utamu wa Yesu we, Si kama nimechanganyikiwa bali ni utamu wa Yesu we, Jamani sijarukwa na akili bali utamu wa Yesu we, Utamu we, nimeonja utamu we x2 Chorus: Utamu we, nimeonja utamu we he x2  Utamu wa Yesu we, Utamu wa Yesu we x2  Utamu we, utamu x3  Utamu wa Yesu we, he  Mwemere, mwemere x4 (?) Viko vingi vitamu lakini mwisho wake mauti, Viko vingi vitamu lakini mwisho wake kilio, Vingine ni vitamu lakini mwisho wake kilio, Ni vitamu lakini mwisho vichungu kama shubiri, Ni vitamu lakini mwisho vinawasha kama upupu, Ni vitamu lakini mwisho vinapalia we, Acheni niuseme utamu wa Yesu we, Wacheni nisifu utamu wa Yesu we, Umetutenga mbali na dhambi, utamu wa Yesu we, Haufanani na utamu wa asali, utamu wa Yesu we, Thamani yake imeshinda almasi, utamu wa Yesu we, Ni mali ghafi isiopatika kwa mapesa jamani ...

13. YESU NAKUPENDA

YESU NAKUPENDA (By Rose Muhando) Chorus: Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda x2 Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda, Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda, Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda, Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda, Yesuuuu, yesu. Msalabani dhambi zangu ulichukua, Kufika kalivari Bwana ulizitua Nami niwekwa huru ninakwimbia. (Repeat) Nikufananishe na nani mwokozi wangu? Naona fahari mimi ninakuimbia, Nani asimame badala yako? Hakuna mwingine ni wewe pekee yako. (Repeat) Nafahamu Yesu anipenda mimi. Chorus: Yesu wee nakupenda, bwana yesu wee nakupenda,x2 Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda, Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda, Kama vile wewe ulivyo nipenda kwanza nakupenda, Kisha tena ukautoa uhai wako nakupenda, Yesuuuu, yesu. Nilipokuwa kwa shetani niliugua, Ndugu na jamaa zangu walinikimbia, Lakini yesu wa huruma ukanihurumia, Nikufananishe na nani mwokozi wangu? Naona fahari mimi ninakuimbia, Nani asimame badala yako? Ha...

14. WANYAMAZISHE

WANYAMAZISHE (By Rose Muhando) Wanyamazishe bwana Milele wanyamaze Wafunge mpito kwa Yesu Na wakae kimya kimya Wanyamazishe bwana Wanyamaze Wafunge mpito kwa Yesu Na wakae kimya kabisa Wapofushe macho yao Wasinione wakae mbali nami Ah wasinione Kwa kuwa walitangaza msiba juu yangu Wala hawakutaka ipone nafsi yangu Wakafanya sherehe kupitia jina langu Waliona fahari kutangaza mauti yangu Wakachuma na pesa kupitia jina langu Hawakuona vibaya kuumiza familia yangu Walifanya dhihaka kudhihaki watoto wangu Ah namtuma malaika nyumbani kwao Atangaze msiba kwenye familia zao Namtuma Gabrieli malangoni kwao Atangaze msiba malangoni kwao Nawafanye matanga maishani mwao Natangaza msiba kwenye malango yao Natangaza matanga nyumbani kwao Yasikome matanga kwenye familia zao Laana kifo, iwe juu yao Wala wasiwe salama watoto wao Mauti iwe fungu lao Kushindwa uwe mbele yao Kwa kuwa mimi nimekutumaini Wanyamazishwe Watahayarishwe, wafedheishwe Wahangaike, waaibike Kwa kuwa mimi nimekutumaini Wanyamazish...

15. KENYA ULINDWE

KENYA ULINDWE (By Rose Muhando) Shukurani zangu kwa taifa la Kenya Viongozi wa Kenya Na wananchi wa Kenya Kwa kuokoa maisha yangu (Jawabu Studios) Uhuru, baba Uhuru We Uhuru, yabarikiwe malango yako Uhuru, baba Uhuru We Uhuru, yabarikiwe malango yako Kenya Kenya, ulindwe Ulindwe, Kenya ulindwe Milele ulindwe Ifanikiwe mipaka yako Ulindwe, Kenya ulindwe Milele ulindwe Ifanikiwe mipaka yako Malango yangu ulifungua Mikononi ukanipokea Kenya ukanihurumia Yabarikiwe malango yako Mikono yako ulikunjua Ukanisaidia Kenya ukanihurumia Yafanikiwe malango yako Cha kukupa sina Mali sina Chochote sina Ubarikiwe malango yako Uwezo sina Mali sina Nakuombea kwa Mungu Baba Yabarikiwe malango yako Uhuru, baba Uhuru Rais Uhuru, yabarikiwe malango yako Narudia Uhuru, tena Uhuru Wewe Uhuru, ifanikiwe mipaka yako Kenya, ulindwe Kenya, ulindwe Kenya, ifanikiwe mipaka yako Uhuru, baba Uhuru We Uhuru, yabarikiwe malango yako Uhuru, baba Uhuru We Uhuru, yabarikiwe malango yako Kenya Kenya, ulindwe Ulindwe, Keny...