14. WANYAMAZISHE

WANYAMAZISHE
(By Rose Muhando)

Wanyamazishe bwana
Milele wanyamaze
Wafunge mpito kwa Yesu
Na wakae kimya kimya
Wanyamazishe bwana
Wanyamaze

Wafunge mpito kwa Yesu
Na wakae kimya kabisa
Wapofushe macho yao
Wasinione wakae mbali nami
Ah wasinione

Kwa kuwa walitangaza msiba juu yangu
Wala hawakutaka ipone nafsi yangu
Wakafanya sherehe kupitia jina langu
Waliona fahari kutangaza mauti yangu
Wakachuma na pesa kupitia jina langu

Hawakuona vibaya kuumiza familia yangu
Walifanya dhihaka kudhihaki watoto wangu
Ah namtuma malaika nyumbani kwao
Atangaze msiba kwenye familia zao
Namtuma Gabrieli malangoni kwao

Atangaze msiba malangoni kwao
Nawafanye matanga maishani mwao
Natangaza msiba kwenye malango yao
Natangaza matanga nyumbani kwao
Yasikome matanga kwenye familia zao

Laana kifo, iwe juu yao
Wala wasiwe salama watoto wao
Mauti iwe fungu lao
Kushindwa uwe mbele yao
Kwa kuwa mimi nimekutumaini
Wanyamazishwe

Watahayarishwe, wafedheishwe
Wahangaike, waaibike
Kwa kuwa mimi nimekutumaini
Wanyamazishe bwana
Milele wanyamaze

Wafunge mpito kwa Yesu
Na wakae kimya kimya
Wanyamazishe bwana
Wanyamaze

Wafunge mpito kwa Yesu
Na wakae kimya kabisa
Wapofushe macho yao
Wasinione wakae mbali nami
Ah wasinione

Ah Mikaeli wa vita namtuma kwao
Upeleke mafarakano kwao
Wasielewane waupwa wao
Nasema wagombane wauma wao

Walane watafunane waupwa wao
Wavurugane waupwa wao
Maadui wapigane waupwa wao
Mungu mwenyezi awe adui wao

Wakitazama kulia wamwone Gabrieli
Wakitazama kushoto wamwone Micaeli
Mbele yangu wamwone Rafaeli
Wafadhaike

Watahayarishwe
Wagonganishwe
Watayarike usiwape nafasi
Wanyamazishe bwana
Milele wanyamaze

Wafunge mpito kwa Yesu
Na wakimyee milele
Wanyamazishe bwana
Wanyamaze

Wafunge mpito kwa Yesu
Na wakae kimya kabisa
Wapofushe macho yao
Wasinione wakae mbali nami
Ah wasinione.

Comments

Popular posts from this blog

03. NYOTA YA AJABU

07. NAKAZA MWENDO

04. SITANYAMAZA