Posts

01. MUNGU WA MAPENDO

MUNGU WA MAPENDO (By Rose Muhando) [Nini kitanitenganisha ( Na upendo wa Mungu Baba), Ikiwa ni dhiki au njaa (Havitananitenga naye Baba), Mauti, upanga, na dhihaka (Havitananitenga naye Baba) ] x2 Chorus: [Sina hofu sibabaiki, Kwake yeye nime/nitashinda, Milele yote nime/nitashinda, Tena zaidi ya kushinda, Kwake yeye aliyenipenda] x2 Kwenye zamu yangu nitasimama,  Kwa miguu yangu nitasimama, Nione Bwana atakavyonijibu mimi, Kwa habari ya kulalamika kwangu, Bwana aliniambia neno hili, “Usiogope maneno yao, Usitetemeke mbele yao, usifadhaike mbele yao, Maana imeandikwa, kwa ajili yako ninauawa, kama kondoo wa kuchinjwa, kifo nimehesabiwa, Kifo nimehesabiwa, mimi sibabaiki. Bridge: Shetani usinisumbue (Shetani usinisumbue) Wala usinibababishe (Wala usinibababishe)  Funga kinywa ukatoweke (Funga kinywa ukatoweke)  Nyamaza kimya ukapotee (Kwa jina la Yesu ukatoweke)  Nyamaza kimya ukapotee (Nyamaza kimya ukapotee). Chorus: [Sina hofu sibabaiki, Kwake yeye nime/nitashind...

02. NIBEBE

NIBEBE (By Rose Muhando) Chorus: Nibebe nibebe nibebe nibebe, Nibembeleze nibebe, Nichukue unibebe, Mikononi mwako niwe salama. Verse 1: E mungu angalia kunena kwangu,  Na usikie sauti ya kilio changu, Moyo wangu umechoka sana baba,  Kwa ajili ya wingi wa mateso yangu, Nafsi yangu imegandamana na mavumbi, Niokoe mikononi mwa midomo ya mbwa, Kwanini ninateswa sana kwa ajili yako babangu? Niokoe mikononi mwa watu wabaya, fanya hima unisaidie nibebe. Chorus: Nibebe nibebe nibebe nibebe, Nibembeleze nibebe, Nichukue unibebe, Mikononi mwako niwe salama. Nimechoka peke yangu safari ngumu ni ndefu nibebe. Chorus: Nibebe nibebe nibebe nibebe, Nibembeleze nibebe, Nichukue unibebe, Mikononi mwako niwe salama. Verse 2: Macho yangu yamedhoofukwa machozi, Kwani mateso yangu hayapimiki kwa mizani, Kwa kuwa aliyenitukana siye adui yangu, bali ni rafiki yangu tuliyejuana naye sana, Tulikula pamoja, tulisali pamoja, kanisani pamoja, Bwana asifiwe kwa sana, Kumbe mwenzangu alikusudia kuniangami...

03. NYOTA YA AJABU

NYOTA YA AJABU (By Rose Muhando) Verse 1: Ile nyota ya ajabu, yaonekana mashariki Imejaa ishara zote, za kuzaliwa mfalme Mamajuzi wako nyuma, kuifuata nyota ile walifika Yerusalemu, nao wakauliza (Repeat) Yuko wapi yeye aliyezaliwa, mtawala wa wayahaudi ili tumsujudie. Chorus: Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi Atakayewaokoa watu na dhambi zao Dunia shangilieni, amezaliwa messiah Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana. Verse 2: Walikuwako na wachungaji, waliokaa makondeni Wakilinda kundi lao kwa zamu usiku Malaika kawatokea, kawambia msiogope Maana leo katika Yuda, amezaliwa messiah. Chorus: Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi Atakayewaokoa watu na dhambi zao Dunia shangilieni, amezaliwa messiah Haleluya haleluyah, sifa ni kwa Bwana. Verse 3: Walipokwisha kusema haya, Malaika wa bwana Waliimba wimbo ule, wimbo usio na mwisho Utukufu juu kwa Mungu mbinguni Duniani we amani kwa aliowaridhia. Chorus: Mjini mwa Daudi, amezaliwa mkombozi Atakayewaokoa watu na dhambi zao Dunia shangilieni, a...

04. SITANYAMAZA

SITANYAMAZA (By Rose Muhando) Eeeehhhh! Mimi Mungu (Me, God) Matendo nitalia, Kwa sinani nitaomboleza Sodoma nitanung'unika, Mipakani nitashambulia Mijini wameniacha,Kila mara nitashambulia Maisha ya wanadamu, Yamenichosha! Oh oh mimi Sitanyamaza, wala sitanyamaza Lakini nitalipa ujira wa vifuani mwao Maovu yenu ninyi, pamoja na baba zenu nasema nitalipa ndio mjue mimi ni Bwana Mmefukiza uvumba, na kunitukana Kwa ajili ya haya mtajutia vitani mwenu? (repeat) Mmefanya uzinzi katikati ya milima Usiku wa manane mmefanya ukahaba Kwenye njia kuu na vichochoro mmefanya mapatano Kwenye mialoni na mipera mmefanya machukizo. (repeat) Ulitumaini uzuri wako ukafanya ukahaba Kila kijana aliyepita ulimwona anafaa Awe mzuri na sura mbaya ulifunua marinda. Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda Wako wapi mapenzi zako mbona sasa unakonda Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda Wako wapi waelizamu (?) wako mbona sasa unakonda. Miji mizuri imekuwa ukiwa Majumba mazuri yamefungwa kabisa Wana w...

05. UTUKUZWE

UTUKUZWE (By Rose muhando) Ee Mungu utukuzwe, milele na milele, Tena uinuliwe, katika mataifa yote, Ee Mungu utukuzwe, milele na milele, Ee Mungu uinuliwe, milele na milele, Tena uhimidiwe katika mataifa yote, Jina lako la ajabu, Wewe utishaye kuliko x2 Wala haufanananishwi na chochote, Jina lako Baba la ajabu. Refrain: Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika), Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia), Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania) Wakafika (Kule Kanaani salama) x2 Usifiwe, utukuzwe x2 Utukufu ni wako, milele na milele x2 Haya visiwa na viimbe,  Mito na ipige makofi, Ndege na waseme amina kubwa, Wanyama wa mwitu wasifu x2 Bwana anatawala/Maana unatawala, wewe Bwana, Heshima na enzi ni vya Bwana, Utukufu na nguvu ni vya Bwana, Umeketi mkono wenye nguvu  x2 Refrain: Wewe uliupiga mwamba  (maji yakabubujika), Katikakati ya jangwa  (wewe ulifanya njia), Walipokumbana na adui  (Wewe uliwapigania) Wakafika  (Kule Kanaani salama)  x2 Usifiwe, ut...

06. KIATU KIVUE

KIATU KIVUE (By Rose Muhando) Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue, Mungu alinena naye Musa hicho kiatu kivue, Ulichotoka nacho kwa farao nakwambia, Pahali hapa ni patakatifu hicho kiatu kivue (x2) Musa hicho kiatu, Musa hicho kiatu, Nataka ninene nawe, nataka nikutumie, Nataka nikuinue, nataka nikubariki, Watu wangu waangamia,taifa langu la Israeli, Watu wangu wanasononeka,watu wangu wanateseka, Nataka nikutumie wewe, ukaokoe taifa langu we. Hata leo mungu anena nasi hicho kiatu we, Kiatu ni dhambi uzifanyazo ninakwambia, Ukahaba unaoeneza kando kando ni kiatu, Wivu na masengenyo vimekuja ni kiatu, Kitakupeleka jehanamu hicho kiatu, Kitakupeleka motoni wewe hicho kiatu, Uzinzi unaoeneza wewe ni kiatu, Uvalie wake wa wenzio magoti we nakwambia, Utongoza waume wa wenzio ni kiatu we, Kitakupekea jehanamu hicho kiatu, Mama hicho kiatu, baba hicho kiatu, Nataka ninene nawe, maana ninakupenda, Nataka ninene nawe, ili nikuokoe, Mimi sitaki uangamie, mimi sitaki upotee, Mimi sitaki uanga...

07. NAKAZA MWENDO

NAKAZA MWENDO (By Rose Muhando) Verse 1: Nafurahia mateso yangu, nafurahia mateso yangu, Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba, Ujapoharibika mwili huu, tapata mwingine kwa Baba. Chorus: Nakaza mwendo, nifike Mbinguni, Nayakabidhi, maisha kwa Bwana, Nauone, uzuri wa bwana x2 Taabu na matatizo, hakuna, Kiu wala njaa, hakuna x2 Verse 2: Lakini mji ule taa yake, ni mwana kondoo, Milele mji ule hauitaji, jua wala mwezi. Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida. Chorus: Nakaza mwendo, nifike Mbinguni, Nayakabidhi, maisha kwa Bwana, Nauone, uzuri wa bwana x2 Verse 3: Lakini waongo na wazinzi, hawataingia, wala waabudu sanamu, hawataingia x2 Najua kuishi kwangu ni pigo, kufa ni faida. Chorus: Nakaza mwendo, nifike Mbinguni, Nayakabidhi, maisha kwa Bwana, Nauone, uzuri wa bwana x2