05. UTUKUZWE

UTUKUZWE
(By Rose muhando)

Ee Mungu utukuzwe, milele na milele,
Tena uinuliwe, katika mataifa yote,
Ee Mungu utukuzwe, milele na milele,
Ee Mungu uinuliwe, milele na milele,
Tena uhimidiwe katika mataifa yote,
Jina lako la ajabu, Wewe utishaye kuliko x2

Wala haufanananishwi na chochote,
Jina lako Baba la ajabu.

Refrain:
Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika),
Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia),
Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania)
Wakafika (Kule Kanaani salama) x2
Usifiwe, utukuzwe x2
Utukufu ni wako, milele na milele x2

Haya visiwa na viimbe, 
Mito na ipige makofi,
Ndege na waseme amina kubwa,
Wanyama wa mwitu wasifu x2
Bwana anatawala/Maana unatawala, wewe Bwana,
Heshima na enzi ni vya Bwana,
Utukufu na nguvu ni vya Bwana,
Umeketi mkono wenye nguvu  x2

Refrain:
Wewe uliupiga mwamba (maji yakabubujika),
Katikakati ya jangwa (wewe ulifanya njia),
Walipokumbana na adui (Wewe uliwapigania)
Wakafika (Kule Kanaani salama) x2
Usifiwe, utukuzwe x2
Utukufu ni wako, milele na milele x2

Heshima ni yako (milele na milele),
Utukufu ni wako (milele na milele),
Heshima ni yako (milele na milele),
Mamlaka ina wewe (milele na milele),
Malaika waimbe (milele na milele),
Wazee ishirini na nne waseme (milele na milele),
Na wale wenye uhai waimbe (milele na milele),
Na watakatifu waseme (milele na milele).

Comments

Popular posts from this blog

03. NYOTA YA AJABU

07. NAKAZA MWENDO

04. SITANYAMAZA